Find Us Online At
iBookstore
Android app on Google Play
Like Us
A programme by
Kusimama Juu ya Mabega ya Muindaji
22 January 2013

Nyota iliyopo katikati ya picha inaitwa Betelgeuse,ipatikanayo katika mabega ya muindaji mkubwa katika konstilesheni ya Orion. Konstilesheni ni picha katika anga la usiku katika maumbo mbali mbali ya vitu, wanyama na watu ambazo zimetengenezwa kwa kuunganisha nyota, kama fumbo la kuunganisha nukta ili kupata umbo! Orion inaweza kuonekana kwa urahisi kwa kutumia macho, na huonekana katika kizio cha kaskazini wakati wa baridi. Betelgeuse ni nyota yenye rangi ya Chungwa iliyopo upande wa juu kushoto kwa nyota tatu maarufu zinazotengeneza mkanda wa muindaji. Unaweza kutoka nje usiku wa leo ili kujionea mwenyewe! 

Katika picha hii, Betelgeuse inaweza kuonekana ni ndogo lakini ni Red Supergiant yenye ukubwa karibu mara 1000 zaidi ya Jua letu na inang’aa mara 100,000 zaidi! Lakini muonekano wake huu wa kupendeza una gharama zake pia. Betelgeuse inakaribia kufa, tena kifo cha mlipuko mkubwa na wenye nguvu uitwao Supernova. Angalia pichani, unaweza kuona imeshaanza kupoteza baadhi ya maada zake katika tabaka la nje! 

Kama ilivyo kwa Jua, Betelgeuse ilikuwa ni nyota ya kawaida tu. Ila imezeeka kuvimba na kuwa kubwa, hivyo kuanza kushindwa kuhimili matabaka yake ya nje na kutawanya maada zake huko angani. Maada ambazo zimetengeneza nusu duara, ambalo unaweza kuliona katika picha likiwa limejikunja katika upande wa kushoto wa nyota. 

Ukiweza kuangalia kwa ukaribu, unaweza kuona pia kitu cha kushangaza, mstari ulionyooka wa maada katika upande wa kushoto wa picha. Wanasayansi wanaamini kuwa mstari huu hauna uhusiano wowote na nyota. Unaonekana kama ni ukingo wa wingu jeusi la vumbi na gesi ambalo limemulikwa na mwanga wa Betelgeuse. Kama wanachofikiria ni sawa, inaonekana kuwa Betelgeuse inaelekea kugongana mda si mrefu!

Dokezo

Ukilinganisha na umbali wa angani nyota ya Betelgeuse ipo karibu sana na Dunia. Hii inamaanisha kuwa ikilipuka katika supernova, itaonekana vizuri sana kwani itawaka kama mwezi unavyowaka angani!

Share:

More news
12 October 2020
1 October 2020
16 September 2020
14 September 2020
10 September 2020

Images

Standing on the Shoulders of Giants
Standing on the Shoulders of Giants

Printer-friendly

PDF File
972.2 KB