Find Us Online At
iBookstore
Android app on Google Play
Like Us
A programme by
Shimo Jeusi katika ya Vumbi
20 June 2013

Karibia kila galaksi ina shimo kubwa kati kati yake. Mengine yamekaa kimya katika kiza yakisubiria vitu vinavyoizunguka vilikaribie. Mengine yanafyonza vitu kwa haraka sana hata katika muda huu tunaoongea na kuyafanya yawe na nguvu zaidi kadri yanavyomeza maada nyingi zinazolizunguka. Mashimo haya makubwa yanajulikana kama Mashimo Meusi “Black Holes”, na pale yanapokuwa yanameza kitu hutengeneza mwanga mkali na nishati kubwa katika Ulimwengu: ambazo ni nishati kali za kinyuklia zilizopo angani!

Wakati ambapo shimo jeusi linavuta gesi na vumbi angani, hutengeneza umbo linafanana na donati, au kama maji yanapovutwa kwenye sinki. Mzunguko huo huzunguka kwa haraka zaidi kadri unavyoingia ndani na kufanya jotoridi kupanda na kuwa kubwa mno. Wakati hili linatokea, matabaka yanayolizunguka hutoa kiasi kikubwa cha nishati ya mwanga ambayo hunaswa na darubini zetu.

Wakati tunaangalia moja ya vyanzo vikubwa hivi vya nishati, tulitegemea kuona shimo kubwa jeusi katika kiini cha nyota kubwa yenye joto, kuelekea ndani. Hatutegemei shimo hili kujificha katika mavumbi ya angani. Ingawa hicho ndicho kilichoonwa wakati wa kuchunguza shimo jeusi lenye nguvu! Gimba la vumbi lenye joto la kawaida, ambalo ni joto dogo zaidi kulinganisha na vumbi lingine linlolizunguka lenye jotoridi la 700 Celsius! Vumbi hili limetokana na upepo unaovuma kutoka katika shimo jeusi.

Ugunduzi huu mpya si wa kawaida kwani mashimo meusi huitaji kuvuta maada ili kupata nishati, lakini kwa hili linaonyesha kutumia nishati kubwa iliyozalishwa kupulizwa vitu nje! Kwa sasa hili ni fumbo jingine kuhusiana na mashimo haya meusi ambalo bado halijatatuliwa.

Dokezo

Kama ilivyo kwa vitu vingi vilivyopo Ulimwenguni zikiwamo Sayari, galaksi na nyota, kuna aina nyingi za galactic nyuklia zenye nguvu. Ingawa nyingi hutofautiana kutokana na kule zinapoangalia wakati tunazitazama. Kwa mfano kuna ‘blazars’na ‘quasars’ ambavyo tunaviona chini ya mchirizi. Ingawa ‘Seyferts’ huwa inaangaliwa kutoka katika upande wa mchirizi.

Share:

More news
12 October 2020
1 October 2020
16 September 2020
14 September 2020
10 September 2020

Images

The Greedy Monster in a Dusty Blanket
The Greedy Monster in a Dusty Blanket

Printer-friendly

PDF File
992.5 KB