Find Us Online At
iBookstore
Android app on Google Play
Like Us
A programme by
Volkano ya Zuhura
4 December 2012

Katika Dunia, uji uji unaowaka na kuchuruzika kutoka katika milipuko ya volkano ni moja kati ya mambo makubwa yenye nguvu na kustaajabika ya kiasili. Na sasa wanaastronomia wameweza kugundua kwamba milipuko ya volkano inatokea kwa kasi hata kwenye Zuhura (Venus), sayari iliyo karibu kabisa na Dunia.

Katika mwaka 2005, wanaastronomia walituma chombo kilichoitwa Venus Express ili kuichunguza sayari ya Zuhura kwa ukaribu. Chombo hicho kimekuwa kikizunguka katika obiti ya Zuhura tangu wakati huo. Kwa bahati mbaya hali ya hewa kwenye Zuhura ni ya mawingu  karibu mda wote na kuifanya sayari hii ifunikwe na mawingu, na kukifanya chombo kisiweze kuangalia moja kwa moja volkano zilizopo katika uso wa Zuhura. Hivyo wanaastronomia wakaamua kutumia ujanja; na kutafuta gesi maalum ambayo huwa inatolewa pale volkano inapokuwa imelipuka. Gesi hii kuna wakati ambapo huwa inaonekana katika wingu zito la Zuhura na kufanya Venus Express iweze kuiona. Kwa kutumia chombo hicho, waliweza kuona mabadiliko makubwa ya kiwango cha gesi katika mawingu. Hivyo kuwafanya wafikilie kuwa gesi hizi zinatoka katika milipuko ya volkano.

Katika kipindi cha nyuma, Venus express pia iliweza kupata dodoso za kuwepo kwa volkano. Kwa kutumia kamera maalum inayoweza kuona katika mawingu na kuangalia tofauti ya jotoridi. Kwa kutumia kamera hii ileweza kugundua kitu kilichoonekana kama uji uji wa volkano unaotembea. Hii inaonyesha kuwa jirani yetu sio tu ana hali ya hewa mbaya yenye dhoruba nyingi na joto kali bali pia ardhi yenye inatokota.

Dokezo

Zuhura ni moja kati ya vitu vinavyong’aa sana angani. Lakini huwa inaonekana katika mda fulani tu na kwa kipindi kifupi; kabla ya mawio (angalia upande wa mashariki) au kabla ya machweo (angalia upande wa magharibi).

Share:

More news
12 October 2020
1 October 2020
16 September 2020
14 September 2020
10 September 2020

Images

Volcanic Venus
Volcanic Venus

Printer-friendly

PDF File
1.0 MB