Find Us Online At
iBookstore
Android app on Google Play
Like Us
A programme by
Ni Vipi Utaonekana
20 March 2013

Tukirudi nyuma mwaka 1999 galaxi hii ilikuwa inaelea kwa utulivu na hakuna aliyekuwa anaijali hapa Duniani. Ghafla utulivu huo uliondolewa na mlipuko wa kupendeza. Ilikuwa in kifo cha nyota iliyokuwa kubwa, ambao ni moja kati ya matukio yenye nguvu sana ya asili. Tunaiita milipuko hii Supanova, ambapo mlipuko huu ulitoa mwanga mwingi wa kupita hata ule wa galaxi nzima pamoja na wenyewe.

Muonekano huu wa kushangaza wa galaxi iliyopo karibu nasi ulinaswa na wanaastronomia waliokuwa wanasoma madhara baada ya mlipuko. Waliona mng’ao wa supanova unafifia kadri miaka inavyozidi kwenda. Ulififia kiasi kuwa ile supanova iliyokuwa inaonekana kwa urahisi, ilikuwa haionekani tena kwa urahisi kwenye hii picha. Ijapokuwa supanova hii imefifia sana wanaastronomia waliweza kupata taarifa chache kuhusiana na nyota iliyolipuka. Ambayo ilikuwa kubwa sana kabla ya kifo chake — ukubwa wa zaidi ya mara nane ya Jua!

Picha hii inaweze isionyesha mwanga unaong’aa wa supanova, lakini inaonyesha baadhi ya taarifa muhimu. Galaxi hii inajulikana kama ‘spiral galaxi’ kama ilivyo kwa Milky Way. Zimepewa jina hilo kwa sababu ya mbo lake linalofanana na kisahani chenye mikoni mirefu iliyoshikizwa katika kiini cha galaxi hii. Mikono ya galaxi katika picha imekolezwa na sehemu za rangi ya blue zenye nyota changa, gesi zinazowaka na magimba yenye giza.

Dokezo

Supanova moja inaweza kutengeneza nishati nyingi kuliko ile inayoweza kutengenezwa na Jua katika maisha yake yote. Na Jua letu litaishi miaka inayokaribia bilioni 10!

Share:

More news
12 October 2020
1 October 2020
16 September 2020
14 September 2020
10 September 2020

Images

How to Stand Out from the Crowd
How to Stand Out from the Crowd

Printer-friendly

PDF File
1017.1 KB