Find Us Online At
iBookstore
Android app on Google Play
Like Us
A programme by
Nyota Zilizostaafu na Kinyago!
8 November 2012

Mara nyingi watu wakistaafu huchukucha fani mpya ili kufidia mda wao, kama vile kuchora au kuvua samaki. Wanaastronomia katika siku za karibuni wameziona nyota mbili zilizostaafu ( ziitwazo mbilikimo weupe), katika kiini cha nebula ya kupendeza iliyochukua sura ya kinyago! Maada za rangi nyekundu zinachochirizika kutoka katika kila kona ya nebula hii zimejikunja katika mfumo wa S baina ya nyota hizi mbili za zamani. 

Nyota kama Jua ikiishiwa nishati, inaanza kubomoka ndani kwa ndani. Maada zilizopo katika kiini chake huishia kugandamizwa katika tone dogo lenye uzito mkubwa. Tone hili dogo huitwa mbilikimo mweupe. Nyota hiyo pia hupoteza gamba lake la nje la gesi,na kuelea angani. Gesi ambazo hutengeneza planetari nebula – ambayo ni mawingu ya kupendeza yanayozunguka mbilikimo mweupe, kama yalivyoonyeshwa katika picha. 

Sio jambo lililozoeleka kwa wanaastronomia kuziona nyota mbilikimo nyeupe zikiwa zinazungukana katika mfumo unaoitwa mfumo pacha na wanaastronomia. Pia ni aghalabu sana kwa nyota hizi kuwa karibu karibu sana! Wanaastronomia wanatarajia nyota za mbilikimo weupe kuchukua miongo kadhaa ili kukamilisha mzunguko mmoja kuzungukana, lakini kwa hizi mbili huchukuwa muda wa kama siku moja hivi! 

Kadri nyota hizi zinavyozidi kuzungukana, huathiri utupwaji wa maada kutoka katika kiini chake, na kuzisababisha kujipinda katika upo la kuvutia la S.Wanaastronomia wametumia miaka mingi wakistaajabu ni kwa jinsi gani michirizi hii ya kupendeza inavyotengenezwa na sasa wameweza kujua! 

Dokezo

Kipande cha mbilikimo mweupe chanye ukubwa na donge la sukari kinaweza kuwa na uzito sawa na kiboko! 

Share:

More news
12 October 2020
1 October 2020
16 September 2020
14 September 2020
10 September 2020

Images

Retired Stars Take Up Sculpting!
Retired Stars Take Up Sculpting!

Printer-friendly

PDF File
1.0 MB